Starmer akutana na Abbas jijini London
9 Septemba 2025Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amemkarbisha rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina Mahmoud Abbas katika makazi yake jijini London huku serikali ya Uingereza ikipiga hatua kuelekea kulitambua dola la Palestina.
Abbas ameipongeza ahadi ya Starmer ya kuitambua Palestina kabla kufanyika mkutano wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York baadaye mwezi huu ikiwa Israel haitabadili mkondo wa mambo.
Viongozi hao wawili wamekubaliana hakutakuwa na jukumu lolote kwa Hamas katika utawala wa siku za usoni wa Palestina.
Pia wamejjadiliana juu ya hali isiyovumilika katika Ukanda wa Gaza, huku Starmer akisisitiza umuhimu wa suluhisho la haraka kufikisha mwisho mateso na njaa, kwa kuanzia na usitishaji vita, kuachiwa kwa mateka na kuongeza kwa kiwango kikubwa misaada ya kibinadamu.