SPD tayari kwa mazungumzo ya 'dhati' na CDU
26 Februari 2025Matangazo
Klingbeil aliyechaguliwa Jumatano amesema ni matamanio ya SPD kuona kwamba Ujerumani inakuwa na serikali inayofanya kazi mapema iwezekanavyo, ingawa anamuachiajukumu Merz, kufanikisha hilo. "Ninajua jukumu tulilonalo kama Social Democrats, kuifanya nchi hii kuwa imara na kuhakikisha tunakuwa na serikali yenye uwezo.
Hayo pia ni matamanio ya SPD tunapoingia kwenye mazungumzo sasa. Lakini pia ni juu ya Friedrich Merz kulifanikisha hili. Tuko tayari kwa mazungumzo ya dhati, sahihi na mazito. Sasa ninatamani kuona upande wa pili una nini.”
Aidha amesema wana nia ya kuliimarisha jeshi la Ujerumani, Bundeswehr na kuhimiza uwekezaji zaidi kwenye uchumi, wakati mazungumzo baina ya CDU na SPD yakitarajiwa kuendelea.