Somalia yazindua daftari la wapiga kura
16 Aprili 2025Matangazo
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 50, raia wa Somalia walijitokeza kujiandikisha kuwa wapiga kura katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwaka ujao.
Rais Hassan Sheikh Mohamud mwaka jana aliahidi kuufikisha mwisho mfumo wa uchaguzi unaozingatia koo za kikabila ambao ulikuwa ukiwanyima haki raia kuchagua moja kwa moja viongozi wanaowataka.Soma pia: Viongozi wa Somali wakabiliwa na waranti za kukamatwa
Mfumo huo wa uchaguzi umekuwa ukifuatwa tangu mwaka 1969 baada ya kuondolewa madarakani dikteta Siad Barre.