Solana kukutana na Larijani kesho kuzungumuzia mzozo wa kinuklea wa Iran
13 Septemba 2006Muakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana na mjumbe wa Iran katika mazungumzo ya mradi wa kinuklia Ali Larijani wanatazamiwa kukutana tena kesho.Habari hizo zimetangazwa na msemaji wa Bwana Javier Solana mjini Bruxelles.Mazungumzo hayo yatafanyika kokote kule barani Ulaya lakini si mjini Bruxelles-msemaji huyo amesisitiza.Mabwana Solana na Larijani waliyataja mazungumzo waliyokua nayo mwishoni mwa wiki mjini Vienna-Austrria kua ni ya maana.Iran imependekeza kusitisha kwa miezi miwili mpango wake wa kurutubisha maadini ya kinuklea.Wanadiplomasia wa mataifa matano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama na Ujerumani waliokutana jana kwenye makao makuu ya shirika la nishati la kimataifa mjini Vienna, wameshindwa kukubaliana juu ya taarifa ya pamoja kuhusiana na mzozo wa mradi wa kinuklea wa Iran.