Leicester yaachana na van Nistelrooy
27 Juni 2025Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid Van Nistelrooy alijiunga naLeicester mnamo Novemba wakati timu hiyo ikiwa katika nafasi ya 16 kwenye jedwali na kumaliza mbio zao wakiwa nafasi ya 18.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 alishinda mechi yake ya kwanza kama mkufunzi lakini hakuweza kuubadili msimu wa Leicester.
"Ruud ameingoza Leicester ikipita katika kipindi kigumu," Leicester ilisema katika taarifa. "Anaondoka kwa heshima na kila mmoja kwenye klabu anamshukuru kwa kujitolea kwake na bidii yake. Tunamtakia kila la heri huko aendako."
Akiwa mmoja wa washambuliaji bora kabisa wa Ligi ya Premier kuwahi kutokea, Van Nistelrooy hapo awali aliiongoza PSV Eindhoven kutwaa Kombe la Uholanzi kama kocha kabla ya kujiunga na timu ya Erik Ten Hag United kama kocha msaidizi.
Alihudumu kama kocha wa muda hapo Old Trafford baada ya Ten Hag kutimuliwa, hadi meneja mpya Ruben Amorim alipochukua usukani.
"Binafsi napenda kuwashukuru wachezaji wa Leicester City, makocha, shule ya soka na wafanyakazi wote ambao nimeshirikiana nao kwa weledi na kujitolea kwao wakati nilipokuwa klabuni," Van Nistelrooy alisema katika taarifa yake.