Sofia. Bulgaria kuondoa wanajeshi wake nchini Iraq.
3 Septemba 2005Matangazo
Serikali ya Kisoshalist nchini Bulgaria imeamua kuwaondoa wanajeshi wake 370 kutoka Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Waziri mkuu mpya wa nchi hiyo Sergei Stanishev amesema kuwa ataendelea na mpango wa hapo kabla wa kuwaondoa wanajeshi wote mwishoni mwa mwaka huu, akiondoka katika ahadi ya hapo kabla wakati wa kampeni ya kuwaondoa wanajeshi wote mara watakapoingia madarakani.
Amesema kuwa Bulgaria itaanza mazungumzo ya kuwaondoa wanajeshi hao na Marekani pamoja na washirika wengine mwishoni mwa mwezi huu.
Stanishev amesisitiza kuwa Bulgaria inabaki kuwa mshirika mkubwa wa operesheni inayoongozwa na Marekani nchini Iraq.