SiasaIsrael
Smotrich kuelekea Marekani kwa ziara fupi
4 Machi 2025Matangazo
Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X, Smotrich amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Israel na Marekani pamoja na ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.
Soma pia: Türk aikosoa vikali kauli ya Waziri wa fedha wa Israel
Kulingana na Smotrich, katika mikutano yake atasisistiza msimamo thabiti wa Israel katika mapambano dhidi ya ugaidi na haja ya uungaji mkono wa wazi wa Marekani kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kiusalama katika vita.
Smotrich amesema atakutana na Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent, pamoja na maafisa wengine wa serikali ya Marekani.