Sistani aridhia katiba ya Iraq:
7 Machi 2004Matangazo
BAGHDAD: Baada ya mabishano marefu hatimaye kiongozi wa madhehebu ya Kishiya nchini Iraq, Ayatollah Ali as-Sistani ameikubali katiba mpya ya mpito. Katiba hiyo mpya ya mpiti itasainiwa Jumatatu ya kesho, aliarifu mwanachama wa Kishiya wa Baraza la Serikali baada ya mazungumzo yake pamoja na Ayatollah Sistani. Kufuatana na pingamizi zake dhidi ya ibara mbili, utiaji saini ulibidi uakhirishwe dakika ya mwisho hapo Ijumaa. Kufuatana na mbinyo wake wanachama wa Kishiya katika Baraza la Serikali walipinga ibara inayozingatia kuwapa madaraka zaidi Wakurdi na kutia maanani mpango wa kuundwa Baraza la Rais kutoka kiongozi wa taifa na wawakilishi wake wawili. Taarifa kutoka Baghdad ilisema Wakurdi na Wasunni walipinga kufanyiwa mabadiliko hati ya katiba hiyo.