Simba SC yaendelea kupambana ligi kuu Tanzania
5 Mei 2025Simba anaingia katika mchezo huu akiwa hana cha kupoteza na endapo atapata sare au kufungwa basi Mbio za kutwaa Ubingwa ataanza kuziaga
Katika Mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba alifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 dhidi ya JKT Tanzania
Kocha Msaidizi wa Kikosi cha Simba Suleman Matola ''Tuna wakati mgumu kila baada ya siku 2 tunacheza mechi kwa hiyo ratiba imekuwa ni ngumu kwetu sisi lakini tunamshukuru Mungu baada ya mechi ya juzi hatujakuwa na majeruhi yoyote naimani katika nafasi zitakzopatikana zitageuzwa kuwa magoli"Alisema Suleman Matola
"Mchezo hauwezi kuwa rahisi kama mzunguko wa kwanza mchezo ulikuwa mgumu na hasa saivi ukizingatia michezo ni ya mzunguko wa mwisho kila Timu inajidhatiti kufanya vizuri tunajua kabisa mchezo hauwezi kuwa rahisi lakini sisi kama simba tuanataka point tatu"Alizema Mchezaji wa Simba David Kameta.
Soma pia: Rais wa Tanzania aipongeza Simba kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika
Kocha msaidizi wa Kikosi cha JKT Tanzania Raymond Dotto"kwenye mchezo kilka mechi ina mpango wake Simba tushakutana mzunguko wa kwanza tulipoteza mchezo huo kwa mkwaju wa Penalt tunachoweza kukisema tumejiandaa kukabiliana nao kwa namna watakavyokuwa"Alisema Raymond Dotto.
"Sisi kama wachezaji tumekaa tumekubaliana kwamba kila mtu katika nafasi yake ajitahidi hauwezi kutokufanya makosa ila tupunguze yale makosa makubwa ambayo yanaweza kutugharimu" Alisema Hassan Kapalata Mchezaji wa Jkt Tanzania.
Je, ni JKT Tanzania ama Simba SC?
Mchambuzi wa Soka Justine Mhalinga kuhusu Nafasi ya simba katika Mbio za ubingwa. "Aina ya mechi ambazo wanakwenda kucheza ni ngumu sana Mechi dhidi ya Jkt Tanzania,Pamba Jiji Mei 8,KMC M,ei 11 kuna ugumu namna ambavyo watacheza hizi mechi hizi ambazo zimebaki za viporo hususani kikosi chao kimekuwa kikitumika kilekile katika mashindano yote nafasi ni ngumu sana.
"Kwa Simba kuweza kutwaa ubingwa kulingana na jinsi ambavyo Ratiba ilivyo hata nikitazama kwenye msimamo kiongozi wa Ligi ana alama 70 itampasa Simba ashinde Mechi 3 afikishe alama 69 kwa hiyo Simba wanawakati Mgumu sana"Alisema Mchambuzi wa Soka Justine Mhalinga.
Yanga anaongoza Ligi kuu kwa alama 70 za mechi 26 akiwa amesaliwa na mechi 4 kukamilisha ligi kuu Tanzania bara Wakati Simba anashika nafasi ya Pili akiwa na Alama 60 za Michezo 23 akiwa amesaliwa na mechi 7 kukamilisha Ligi Kuu.