Sidi Ould Tah achaguliwa kuwa rais mpya wa AfDB
29 Mei 2025Matangazo
Sidi Ould Tah amewashinda wagombea wengine wanne, katika kinyanganyiro hicho cha kuchukua nafasi ya rais wa sasa wa benki hiyo Akinwumi Adesina kutoka Nigeria.
Wagombea hao ni mwanamke kutoka Afrika Kusini Swazi Tshabalala, Amadou Hott wa Senegal, Samuel Munzele Maimbo wa Zambia na Abbas Mahamat Tolli wa Chad.
Benki ya AfDB kuchagua rais mpya
Akinwumi Adesina ataachia ngazi mwezi Septemba, baada ya kutumikia vipindi viwili vya miaka mitano mitano. AfDB ni taasisi kubwa zaidi ya fedha za maendeleo barani Afrika na inamilikiwa na Mataifa 54 ya Afrika na nchi zilizostawi kiviwanda duniani za G7, kama Marekani na Japan.