Siasa ya Israel yalaumiwa na wakuu wake wa kijasusi
15 Novemba 2003Matangazo
JERUSALEM: Nchini Israel viongozi wanne wa zamani wa Shirika la Kijasusi Shin Bet wamelaumu vikali siasa ya serikali. Katika mahojiano waliofanyiwa na gazeti la JEDIOTH ACHORONOTH viongozi hao wanne kwa pamoja wanasisitiza kuwa lazima Israel ihamishe makaazi ya Kiyahudi kutoka ardhi za Kipalestina, ikiwa inataka kuishi kwa salama pamoja na Wapalestina. Bila ya kufanywa mkataba wa amani pamoja na Wapalestina, utaendelea kuhatarika usalama wa Israel.