Shughuli za uokozi zinaendelea New Orleans ambako polisi imewataka watu waliosalia majumbani mwao wauhame mji huo.
6 Septemba 2005New-Orleans:
Wiki moja baada ya kimbunga Katrina kupiga kusini mwa Marekani,waokoaji wanaendelea kuingia mitaani huko New Orleans kuwahamisha watu waliofungika majumbani na kukusanya maiti zilizotapakaa majiani.Polisi imewasihi watu waliosalia majumbani mwao watokea,ikionya hakuna maji,hakuna chakula wala ajira kwa waliosalia.Meya wa mjui huo Ray Nagin anasema hatoshangaa kama idadi ya waliokufa New-Orleans kutokana na kimbunga Katrina itapindukia elfu kumi.Hata hivyo amesema hali sasa imeanza kuimarika.Wataalam wanaamini patahitajika hadi miezi mitatu hadi maji yote yatakapokauka.Rais George W. Bush,anaelaumiwa kwa kukawia serikali yake kuingilia kati,analitembelea kwa mara nyengine tena eneo hilo la mizozo.Ameahidi kwa mara nyengine tena misaada ziada kwa wahanga wa kimbunga Katrina.Rais Bush ametangaza hali ya hatari katika majimbo 10-hali itakayoruhusu kutolerwa fedha za shirikisho kusaidia shughuli za uokozi.