Shughuli ya umma kuutazama mwili wa papa yaanza Vatican
23 Aprili 2025Matangazo
Kengele kwenye minara ya kanisa hilo zilipigwa wakati jeneza la kiongozi huyo wa kiroho likisindikizwa na makadinali wakiongozwa na Mwadhama Kadinali Kevin Farrell na walinzi maalum wa Vatican.Soma pia: Papa Francis kuzikwa siku ya Jumamosi mjini Roma
Viongozi wa nchi na serikali duniani wanatarajiwa kushiriki mazishi ya Papa siku ya Jumamosi, lakini shughuli ya kuutazama na kuuaga mwili wa Papa itaendelea kwa siku tatu kuanzia leo Jumatano.Soma pia: Mwili wa Papa Francis wapelekwa Kanisa la Mtakatifu Peter
Kanisa la Mtakatifu Peter litakuwa wazi hadi usiku wa manane leo na kesho ili kuruhusu waumini kuomboleza na shughuli ya kumuaga Papa Francis itamalizika Ijumaa usiku ambapo jeneza lake litafungwa kabisa.