Salaam Charity yabadilisha maisha ya wengi Uganda
19 Agosti 2025Kupitia mitandao ya kijamii kama WhatsApp, wananchi huchangia fedha kidogo kidogo ambazo zikijumlishwa hubadilisha maisha ya wengi. Michango hii imekuwa msaada mkubwa kwa wazee vijijini, yatima, wagonjwa na hata kugharamia miradi ya shule, hospitali na nyumba za ibada. Hajji Abdul-Kareem Kaliisa ni moja wa waasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Salaam Charity.
“Mpango huu ulianza kwa kiwango cha chini tukihamasisha jamii kwamba watu wakiungana kuonyesha upendo miongoni mwetu kuhusu utu tunaweza kupambana na umasikini kama raia wa Uganda. Tunapoendehsa miradi hii inajumuisha kila mtu bila kujiali kabila wala imani. Salaam charity haifanyi hivyo.”
Kwa Salaam Charity, haba na haba hujaza kibaba. Na kwa kila mchango, furaha na matumaini yameendelea kuenea. Na kwa kweli jihihada zao zinapongezwa na wanufaika.
Huu ni uthibitishokuwa misaada ya kiutu si lazima itoke mbali. Hata raia wa kawaida wanaweza kubeba jukumu hilo. Kwa uwazi na uwajibikaji, waasisi wa Salaam Charity wameanzisha pia kituo chao cha televisheni, Salaam TV, ili kushirikisha jamii kinachoendelea, kama anavyoelezea Hajji Kaliisa.
“Tumendelea kuhakikisha kuwa tunatumia idhaa. Tulianzisha Salaam TV kuhakikisha kuwa tunawafikia watu mbalimbali watoe michango ya o kwa sababu hatuwezi kuwafikia wote ana kwa ana kuwakumbusha kutoa michango”.
Katika siku hii ya kuadhimisha misaada ya kiutu duniani, ujumbe wa Salaam Charity ni wazi: misaada ya kibinadamu inaanzia nyumbani, kwa mshikamano wa wananchi wenyewe.