Shirika la NOC lasimamisha shughuli za kiwanda muhimu
15 Desemba 2024Mapigano hayo yamesababisha moto katika hifadhi kadhaa za mafuta.
Katika taarifa yake, NOC ilitangaza hali ya dharura kutokana na uharibifu mkubwa wa matangi ya kuhifadhi mafuta katika kiwanda cha Zawiya, takriban kilomita 45 magharibi mwa Tripoli, uliosababishwa na mapigano hayo.
Ingawa wafanyakazi wa dharura waliweza kuzima moto na kuzuia uvujaji wa gesi, taarifa ziliripoti mtu mmoja kuuawa na wengine 10 kujeruhiwa.
NOC imewahakikishia wakazi wa Zawiya na Tripoli kuwa usambazaji wa mafuta utaendelea bila usumbufu, licha ya changamoto za kiusalama zinazokumba Libya mara kwa mara tangu kuaguka kwa Muammar Gadhafi mwaka 2011.
Kiwanda cha Zawiya, chenye uwezo wa kusafisha mapipa 120,000 kwa siku, ni cha pili kwa ukubwa nchini Libya na kinategemewa kwa usambazaji wa mafuta katika soko la ndani.