Takriban watu 250,000 kote duniani hawajulikani waliko
29 Agosti 2025Matangazo
Shirika hilo limesema idadi hiyo ni ongezeko la karibu asilimia 70 katika kipindi cha miaka mitano. Kutoka Sudan hadi Ukraine, Syria hadi Colombia, vitendo hivyo vinazidi kuongezeka.
Mkurugenzi mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Pierre Krahenbuhl amesema hali hii inaonyesha wazi kwamba watu wamekuwa hawalindwi na pande zinazozozana hasa wakati wa vita.