UchumiKimataifa
IMF yatabiri ongezeko la ukuaji wa uchumi duniani
29 Julai 2025Matangazo
IMF limesema ongezeko hilo la ukuaji wa uchumi linahusishwa na kuimarika kwa shughuli za biashara kabla ya ushuru unaotarajiwa ambao ni mdogo kuliko Marekani iliotishia kuuweka awali.
Sababu nyingine ni kuimarika kwa mazingira ya kifedha na kwa kiasi fulani ni kutokana na sarafu ya dola kudhoofika na hatua za kuimarisha uchumi zilizochukuliwa na mataifa muhimu kiuchumi kama vile China, Ujerumani na Marekani.
Shirika hilo sasa linatazamia kuwa uchumi wa Marekani utakuwa kwa asilimia 1.9 kwa mwaka huu wa 2025 ambalo ni ongezeko la asilimia 0.1 kutoka katika utabiri wake wa mwezi Aprili.