Shirika la akimataifa la nguvu za atomiki linataraji kuitanabahisha Iran ibadilishe fikira
12 Mei 2005Matangazo
Shirika la kimataifa la nguvu za atomiki linataraji juhudi zinazoendeshwa zitasaidia kuishawishi Iran ikubali kurejea katika meza ya mazungumzo kuhusu miradi ya kinuklea.Afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Iran amesema hii leo nchi yake huenda ikaamua kuendelea kwa sehemu na mpango wa kurutubisha maadini ya Uranium kwa sasa.Uamuzi huo ukitekelezwa ,Iran itakua inayaendeya kinyume makubaliano ya November mwaka jana,kati yake,na Uengereza,Ufaransa na Ujerumani.Makubaliano hayo yalilenga kutuliza hofu za walimwengu kwamba Iran inataka kutengeneza bomu la kinuklea.Iran daima aimekua ikishikilia mradi wake huo umelenga matumizi ya kiraia na sio ya kijeshi.