Shinikizo lamfanya Zelenskiy kuwasilisha mswada mpya bungeni
25 Julai 2025Matangazo
Zelenskiy amechukua hatua hiyo katika juhudi za kupunguza mvutano ulioibuka kufuatia hatua yake ya kutia saini sheria yenye utata iliyoziondolea uhuru wa utenda kazi taasisi hizo.
Zelenskiy amesema bunge litaupitia mswada huo, ambao unahakikisha kuimarishwa kwa mfumo wa kisheria wa Ukraine, uhuru wa mashirika ya kupambana na ufisadi na ulinzi wa mfumo wa kisheria dhidi ya uingiliaji wowote wa Urusi.
Mswada wa awali ulidaiwa kuhujumu uhuru wa mashirika hayo na ulipelekea kuzuka kwa maandamano, hayo yakiwa ya kwanza nchini humo tangu Urusi kuanza uvamizi wake.
Umoja wa Ulaya pia ulilaani hatua ya Zelenskiy kuuidhinisha mswada huo.