Shinikizo laongezeka dhidi ya Rwanda na waasi wa M23
26 Februari 2025Ziara hii ikiwa inachukuliwa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kama vile shinikizo dhidi ya Rwanda pamoja na kundi la uasi AFC-M23, inafanyika baada ya umoja wa mataifa pamoja na Umoja wa Ulaya, kuitia kishindo serikali ya Rwanda, kuhusu uungwaji mkono wake kwa kundi la uasi la AFC-M23.
Mjini Kinshasa, Karim Khan alikutana na rais Félix Antoine Tshisekedi, na viongozi hao wawili walizungumzia mauwaji pamoja na vitendo vya uhalifu, vinavyofanywa na waasi katika maeneo waliyoyateka.
Tina Salama ni msemaji wa Rais Félix Tshisekedi, hapa anatupatia matatajio ya serikali ya Congo, kutoka ziara ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC mjini Kinshasa.
Serikali ya Congo ikiwa inatilia maanani tu, visa vinavyoripotiwa katika maeneo yaliyodhibitiwa na waasi wa AFC-M23, mwanaharakati wa Vuguvugu la vijana kwa ajili ya mabadiliko Lucha, Fred Bauma, anamuomba mwendesha mashtaka mkuu wa ICC kuendesha uchunguzi katika maeneo mbalimbali ya Congo, anayoyataja hapa.
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Karim Khan amewaomba wale walio na ripoti kuhusu visa vya mauwaji, kuziwakilisha kwenye anuani ya mtandao wa ICC, ili ripoti hizo zifanyiwe kazi.
Kwa upande wake, Emmanuel Cole, mratibu wa wakfu wa Bill Clinton akitangaza kwamba taasisi yake imepokea kwa furaha ziara ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC mjini Kinshasa, anadhani pia kwamba, uchunguzi wa ICC unapaswa kufanywa kwa ujumla.
Huyu hapa Emmanuel Cole. "Tunasikitika kuona kwamba kuna madhambi upande wa FARDC, wazalendo, ADF na makundi mengineyo mengi. ICC inapaswa kuendesha uchunguzi kwa maswala yote hayo."
Tufahamishe kwamba, Karim Khan anawasili nchini DRC, wakati Rwanda pamoja na kundi la uasi AFC-M23, wanakabiliwa na shinikizo toka jwa jumuiya ya kimataifa, kuiomba Rwanda kuondoa wanajeshi wake Congo, na kundi la uasi AFC-M23 kurudi nyuma.