Shinikizo la jeshi linawaweka mashakani mateka wa Israel
21 Agosti 2025Haya yanafanyika wakati ambapo serikali hiyo inatafakari kuhusiana na pendekezo jipya la kusitisha mapigano hayo yaliyodumu kwa karibu miaka miwili.
Kwa upande wake kundi la wanamgambo la Hamas limesema mpango wa jeshi la Israel wa kuuteka mji wa Gaza City unaonesha wazi kuwa Israel haina nia ya mapigano kusitishwa na kuachiwa kwa mateka katka mzozo huo unaoendelea.
Kwengineko jamaa za mateka ambao bado wanashikiliwa na wanamgambo hao wameandamana katika eneo la mpakani karibu na Ukanda wa Gaza, wakitaka kuachiwa kwa wapendwa wao.
Naye Balozi wa Marekani nchini Israel Mike Huckabee yeye ameyalaumu baadhi ya mataifa ya Ulaya kwa kuvunjika kwa mazungumzo ya amani ya vita hivyo hivi karibuni, akisema hatua yao ya kulitambua taifa la Palestina ndilo lililochngia yote hayo.