Sheria ya kuondoa mbaguano Ujerumani
9 Mei 2006Mada nyengine ni barua alioandikiwa rais Bush wa Marekani na rais wa Iran,Ahmadinejad-rais wa Iran.Sheria ya kupinga mbaguano ilikua mzizi wa fitina ndani ya muungano wa vyama-tawala vya CDU/CSU.Sasa lakini ,mvutano wao umemalizika na uongozi mkuu wa vyama hivyo ndugu umependekeza kwa serikali ya muungano ya Ujerumani kutunga sheria hiyo.
Gazeti la OSTTHÜRINGER ZEITUNG limegundua kwamba, hii ni sheria ile ile ya zamani inayoletwa sasa chini ya mfumo mpya.Laandika:
“Sheria ya kumtendea kila mmoja sawa na bila kumbagua, ni ngao mkononi mwa serikali.Kwani, haivumilii iwapo makazini na viwandani binadamu wanabaguliwa ama kwa kuwa wamezeeka,viwete au wana rangi nyengine isiopendeza.
Kwa kuwa serikali iliopita ya muungano wa vyama vya SPD na Kijani iliitung upya ilingane na hali ya sasa,ilitiwa muunda na vyama hivyo viwili vya CDU/CSU vilipokuwa safu ya upinzani.Kwani, si rahisi kwa vyama hivyo kuitikia-amini kinachopitishwa na serikali yao wakati vilipokuwa upinzani viliipinga sheria hiyo.Na hasa kwavile, vinabidi kutekeleza muongozo uliotolewa na Umoja wa Ulaya tena bila ya kigeugeu.”
Ama gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung linauliza:kwanini sheria hii inapindukia kikomo kilichotakiwa na UU ?
Jibu:
“Yafaa kudhani kwamba hili ni jaribio la kuonesha kukiridhia chama cha SPD(mshirika serikalini).
Lakini katika kipindi kilichopita cha utawala,hata chama cha SPD hakikutaka kuelewa kwanini kiungemkono sheria hii ya kupinga mbaguano iliopendekezwa na mshirika wake chama cha KIJANi wakati ule…?”
Ama ggazeti linalotoka mjini humu:Bonner General-Anzeiger pia linaikosoa serikali likiandika:
„Sheria ya kukataza mbaguano ambayo sasa imeafikiwa na serikali ya muungano wa vyama vikuu ya Ujerumani ni mfano barabara wa siasa mbovu.Kwanza Brussels halafu ikafuata serikali ya muungano iliopita ya vyama vya SPD na KIJANI.
Serikali hiyo ilichukua hatua ya kwanza ya kuipitisha sheria hii na kupamba barabara muongozo kutoka Brussels.Sasa chama cha KIJANI hakiko madarakani na vyama vya CDU/CSU vimeingia madarakani, sheria hii imegeuka mada tofauti na ilivyokua.Ni sawa na kusema: Kanisa halihitajia kuhofia kushtakiwa likikataa kumuajiri muislamu.“
Tukigeuza mada, barua aliyoandika rais Ahmadinejad wa Iran kwa rais Bush wa Marekani juu ya ugomvi wao wa mradi wa nuklia, ni swali jengine lililochambuliwa kwa mapana na marefu na magazeti ya Ujerumani hii leo:Gazeti la Ostsee Zeitung kutoka Rostock linajaribu kuagua kwanini rais wa Iran ghafula amechukua mkondo huu:Laandika:
„Baada ya kupita miaka 27 bila mawasiliano ya kibalozi,Teheran imeaiandikia barua Washington.Je, barua ya Ahmadinejad kwa shetani mkubwa –Marekani ni mchezo mwengine wa kiirani kupitisha wakati katika mgogoro wake wa kinuklia na kambi ya magharibi au ni nia ya kweli ya kupunguza muvtano ?
Likijaribu kutoa majibu,Ostsee-zeitun linadai –yote mawili yawezekana.Ndio maana Marekani na washirika wake waendeleze shinikizo lao kwa Iran.juu ya hivyo,kambi ya magharibi itapaswa kuipa Iran nafasi kujifuta aibu.Hii haitakuwa bila mwishoe kubidi,laongeza gazeti,kwa Marekani kukaa meza moja kwa mazungumzo na utawala wa mamullah wa Teheran.Na haitawezekana katika mazungumzo hayo kuondoka bila kuiridhia Iran kuwa na haki ya kutumia nishati ya kinuklia –lamaliza gazeti.
Gazeti la NÜRNBERGER ZEITUNG linaiangalia barua ya Ahmadinejad kwa jicho hili:
„Maayataolla walioshangiria mwanzoni chokochoko,sasa balaa lake lililozuka linaanza kuwaunguza na hivyo, wanamuambia mchochezi wao amtulize shetani.Kwa kambi ya magharibi-jibu: huo ndio mkondo barabara wa kufuata….“