Sherehe za kuadhimisha miaka 20 tangu ukuta wa Berlin kuanguka
9 Novemba 2009
Leo ni siku ya furaha hapa Ujerumani, kama mlivosikia katika taarifa zetu za habari. Wajerumani wanaadhimisha miaka 20 tangu kuanguka Ukuta wa Berlin uliokuwa alama ya kugawika Ujerumani katika sehemu mbili.
Wananchi wa Berlin Mashariki na Magharibi walipokusanyika katika lango la Brandenburg asubuhi ya tarehe 10,1989Picha: AP
Matangazo
Ukuta huo ulikuwa ni alama ya kukosekana uhuru wa kutembea, wa kutoa maoni na utawala wa mabavu wa kikomunisti katika Ulaya ya Mashariki. Sherehe za shangwe za leo zimesheheni katika mji wa Berlin, hasa katika Lango la Brandenburg ambako Othman Miraji aliungana nako kwa njia ya simu: