SHENA YA URANIUM YA KONGO KWA IRAN ?
6 Agosti 2006LONDON:
Iran ilijaribu kuagiza madini ya uranium kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa mradi wake wa kinuklia ,lakini shehena hiyo ilizuwia Tanzania kwa muujibu gazeti la SUNDAY TIMES la Uingereza lilivyoripoti k leo likinukuku maafisa wa forodha wa Tanzania.
Shehena kubwa ya madini ya uranium 238 iliokua ikielekea Bandar Abbas nchini Iran, ilizuwiwa hapo oktoba 22,mwaka jana na maafisa wa forodha waliokuwa wakifanya ukaguzi wa kawaida –limeandika gazeti.
THE SUNDAY TIMES-limenukuklu pia ripoti ya UM inayotarajiwa kuzingatiwa karibuni na Baraza la Usalama iliodai hakuna shaka kwamba shehena kubwa ya madini ya uranium 238 ilisafirishwa kutoka migodi ya Lumbubashi huko Jamhuri ya Kide mokrasi ya kongo.
Maafisa wa forodha Tanzania wamesema madini hiyo iligunduliwa imefichwa pamoja na shehena ya madini ya coltan-madini adimu iliokuwa ikipelekwa Kazakhstan baada ya kusafirishwa kupitia Bandar Abbas.
Mjumbe mkuu wa Iran katika mazungumzo ya nuklia Ali Larijani alisema leo , Iran haitasimamisha kurutubisha madini ya uranium kama inavyotakiwa kufanya na azimio la UM.