Sharon alaumu siasa ya Mashariki ya Kati ya Ujerumani:
13 Desemba 2003Matangazo
JERUSALEM: Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon ameilaumu Ujerumani kwa ule mchango wake katika juhudi za amani za Mashariki ya Kati. Bwana Sharon aliliambia gazeti la Kijerumani BILD ZEITUNG anaitaka serikali ya Ujerumani ijizuiye zaidi wakati inapowasiliana na Rais wa Pakestina Yasser Arafat. Bwana Sharon alisisitiza kuwa Israel inaitazamia Ujerumani kuwachukulia hatua wale wanaokuza chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani. Akasema atazingatia tena ile ziara yake aliyoakhirisha ya kuja Ujerumani hapo mwakani. Kwa mujibu wa taarifa za Kipalestina wanajeshi wa Israel wamempiga risasi na kumwua mama wa Kipalestina wakati walipoishambulia gari yake katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.