SHANGHAI.Umoja wa Ulaya waitahadharisha China
10 Juni 2005Umoja wa ulaya umeitahadharisha China kuwa itawekewa kikomo katika viwango vya urasimu iwapo haita punguza mauzo yake ya bidhaa za nguo katika soko la nje.
Kamishna wa maswala ya kibiashara wa umoja wa ulaya bwana Peter Mandelson yuko mjini Shanghai kufanya mazungumzo ya mwisho na waziri wa biashara wa China Bo Xilai.
Bwana Mandelson amesema China ina muda hadi kesho jumamosi kupunguza bidhaa zake aina ya T shirts na kitani ambazo zimepindukia kiwango cha asilimia 7.5 zaidi kwa mwaka au iwekewe viwango vya urasimu.
Waziri wa bishara wa China alisema hapo awali kuwa nchi yake itatetea haki ya kibiashara ya bidhaa zake za nguo kuambatana na sheria za shirika la biashara duniani WTO.
Marekani imeshatia mkazo kwa aina saba za bidhaa kutoka China hatua iliyozua malalamiko makali kutoka Beijing.