Wakati operesheni kabambe za kijeshi dhidi ya waasi kutoka Uganda ADF zikiwa zinaendelea na waasi hao wakiwa wamepoteza baadhi ya ngome zao kubwa, hapo jana ADF walijipenyeza katika mji mdogo wa Kokola ulio kilomita 40 kaskazini mwa mji wa Beni mashariki ya Congo na kuwauwa watu kumi. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu John Kanyunyu kutoka Beni.