Shambulizi la droni lateketeza malori 16 ya UN
22 Agosti 2025Matangazo
Msemaji wa Umoja wa mataifa Daniela Gross amewaambia waandishi wa habari kuwa madereva wote na maafisa waliokuwa wanasafiri na Shirika la Chakula Duniani, WFP, wako salama.
Gross amesema haijawa wazi bado ni kundi lipi lililohusika na shambulizi hilo ambalo ni la pili katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ambalo limezuia msafara wa Umoja wa mataifa kuwasilisha misaada huko North Darfur.
Mapema mwezi Juni, msafara wa WFP na Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto UNICEF, ulishambuliwa wakati ulipokuwa unasubiri kuidhinishwa kuelekea mji mkuu wa North Darfur, el-Fasher, na watu watano wakafariki dunia na wengine kujeruhiwa.