MigogoroIsrael
Shambulizi la Israel laua raia pamoja na waandishi, Gaza
25 Agosti 2025Matangazo
Kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza waliouawa ni wagonjwa waliolazwa kwenye ghorofa ya nne ya Hospitali ya Nasser na juhudi za uokozi zinaendelea.
Mkaazi wa Gaza Shadi Al-Arabi amenukuliwa akiomboleza kufuatia mashambulizi hayo, wakati viongozi wa Israel wakiapa kuendeleza mashambulizi kama ilivyopangwa mapema mwezi huu, wakilenga kuudhibiti Mji wa Gaza.
"Hapana, hatutaondoka. Kivyovyote vile, tutakufa tu, ama leo au kesho, tunakufa. Tutakufa kwenye ardhi yetu, hatuondoki. Kama mti, kwenye hii nchi."
Hiyo ndio hospitali pekee inayoendelea kufanya kazi tangu vita vilipoanza miezi 22 iliyopita, lakini sasa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa na watumishi.