Shambulio la Urusi laua mtu mmoja na kujeruhi wawili Ukraine
2 Machi 2025Mamlaka nchini Ukraine zimesema leo Jumapili kwamba Urusi imefanya mashambulizi ya makombora katika mji wa mashariki wa Ukraine wa Kramatorsk na kuua mtu mmoja na kuwajeruhi watu wawili, taarifa hiyo imeongeza kwamba Urusi ilifanya mashambulizi ya droni 79 katika miji kadhaa usiku kucha.
Kupitia mtandao wa Telegraph, Meya wa mji huo Oleksandr Goncharenk amesema mji huo umekuwa ukilengwa kwa mashambulizi ya droni yanayolenga maakazi ya watu na kufanya uharibifu.
Soma zaidi. Kikosi cha jeshi la Uganda chatwaa mji mwingine DRC
Katika hatua nyingine taarifa ya jeshi la anga la Ukraine katika mtandao wa Telegram imesema imefanikiwa kuzidungua droni 63 kati ya 79 zilizorushwa usiku wa kuamkia leo katika miji kadhaa ya Ukraine.
Hata hivyo, Urusi haijatoa tamko lolote juu ya mashambulizi hayo ingawa pande zote mbili zimekuwa zikikanusha kuwalenga raia katika mashambulizi baina yao.