SHAMBULIO LA ROKETI AFGHANISTAN:
11 Januari 2004Matangazo
KABUL: Duru za kijeshi nchini Afghanistan zimeripoti kuwa kombora lilirushwa eneo la uwanja wa ndege unaotumiwa na vikosi vya Kimarekani mashariki mwa nchi hiyo.Lakini roketi hiyo iliyorushwa juu ya anga ya kijiji kilicho karibu na uwanja wa ndege wa mji wa Khost haijaripuka.Mara kwa mara vituo vya Kimarekani katika sehemu za kusini na mashariki mwa Afghanistan hurushiwa makombora.Katika maeneo hayo wanamgambo wanaoipinga serikali,wamefanya mashambulio mengi dhidi ya vikosi,maafisa wa serikali na hata watumishi wa mashirika ya misaada.